(Ki)Swahili (Uganda)

(Ki)Swahili

Uganda: (Ki)Swahili


MAISHA YAKO HAITAKUWA JINSI ULIVYO
NA: Mwinjilisti Sieberen Voordewind

RAFIKI MPENDWA: HITAJI LAKO NI LIPI?
KUSHUSHWA MOYO: UOGA, UCHUNGU, HUZUNI, MATESO, KUFINYILIWA, KUHUKUMIKA MOYONI NA KUKOSA UTULIVU KATIKA MAISHA YAKO?
JE WEWE NI MGONJWA? NIKO NA UJUMBE MZURI KWAKO.
NIKO NA BIBILIA KATIKA MKONO, KUNA NGUVU ZAIDI YA UWEZO WOWOTE WA ULIMWENGU HUU. NI NENO LA MUNGU: BIBILIA
Bibilia inasema: 'ukaniite siku ya mateso, nitakuokoa na wewee utanitukuza (Zaburi 50:15)
Haya siyo mafundisho ya kanisa la ubatizo, au Kikatoliki, Pentecote, au mafundisho ya kanisa. Lakini ni agano la ahadi kutoka kwa Mungu aishie milele.
Mungu akasema: "Mimi ndimi Bwana nikuponyae" (Kutoka 15:26) Nguvu za Mungu ziko tayari kuponya wewe! Pia Nguvu za Mungu ziko tayari kuwasaidia siku ya leo! Ndio Bibilia inasema, Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, mimi (Yesu mwana wa Mungu) nilikuja ili wewe (nyinyi) na muwe na uzima, kasha wawe nao tele".
(Yohana 10:10)
Hii ni habari njema: nawaletea habari njema rafiki, bibilia inasema, "roho ya Bwana Mungu I juu yangu, kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaokoa walovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. (Isaya 61:1)
Habari njema ni hii: "akusamehe maovu yako yote. Akuponye magonjwa yako yote" (Zaburi 103:3)
Habari njema ni hii: Yesu atakusaidia na iwapo utafanya yale bibilia inasema: soma bibilia: amini bibilia na ufanye yale ambayo inasema.
NENDA KWA YESU NA MAHITAJI YAKO YOTE, NA MAISHA YAKO HAITABAKI JINSI ILIVYO!
Nasema: maisha yako haitabaki jinsi ilivyo" Hallo! Nenda kwa Yesu na Yesu! Nenda na mahitaji, uchungu na dhambi zako. Yesu ndie ukweli na uzima. NDIO YESU ANATAKA KUKUTENDEA MIUJIZA.
Miujiza ni jambo ambalo haliwezi kutendeka kwa uwezo wa mwanadamu. Miujiza sio kazi ya waume au wanawake. Huu ni wakati wako wa miujiza!
Ni wakati wa kufunzwa na Yesu ili upokeee muujiza waki.
Halluluhya! Je uko tayari kuchukuwa muujiza uliyo mkuu?
TAFADHALI OMBA NAMI,
"Bwana Yesu nisamehe dhambi zangu, nimehuzunika kwa ajili ya dhambi zangu, nisafishe na damu ya Yesu Kristo, fungua moyo wangu na ukaingie ndani. Nisafishe na inifanye upya na damu ya Yesu kristo na unikubali kama mwanao. Nimekubali wewe huwa mwokozi na mkombozi wa maisha yangu. Asante Bwana kwa maana ulinifia pale msalabani, kwa niaba ya dhambi zangu. Amina!
Amani! "Bibilia inasema, "damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafishe dhambi yote.." (1 Yohana 1:7b)
Na kwa sasa maisha yako hayatakuwa jinsi ilivyo ikiwa utatembea na Yesu (1 Yohana 1: 5-2, 14/Matendo ya mitume 26:18)
Kwa hivyo na kuombea upako wa kawaida na maombi.
Toa macho yako ya kawaida juu ya hali na utarajie muujiza kutoka kwa nguvu za Mungu. Nguvu za roho mtakatifu katika jina la Yesu.
Ikiwa mahitaji yako namna gani usisahau hakuna jambo gumu kwa wale wanao mwamini Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aishie,
Je, ukotayari rafiki yangu weak mkono wako juu ya huu ujumbe naomba, "Mungu wangu katika jina la Yesu Kristo, ninakuja kwako na huyu mume, mke, kijana na msichana ambae anahitaji, ninakusihi ukamguse mtu huyu kwa nguvu zako takatifu katika jina la Yesu. Bwana mponye Mtu huyu kwa asilimia moja. (100%)
Mponye kutoka juu kichwani hadi miguuni, tunaomba shida zake zote Bwana ukawee kufanya miujiza. Ewe rafiki yangu pokea uponyaji katika Jina la Yesu. Pokea ukombizi kutokana na shida zako zote katika jina la Yesu na ukapokee nguvu za Roho Mtakatifu na upako sasa katika jina la Yesu nakuweka huru, Amen"
"bali alijeruhiwa (Yesu) kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisis tumepona" (Isaya 53:5)
Usisahau Mungu ni mkuu kila wakati hata kuliko mahitaji yako!
Mungu anakupenda.
"basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji (Waebrania 4:16)

Maisha yako haitabaki jinsi yalivyo
Tuma ombi l;a maombi kwa: prayer@voordewind.eu 

Swahili translation: Alfred Musunga
TRANSLATION OF YOUR LIFE WILL NEVER BE THE SAME

SOMA ZAIDI: (KI)SWAHILI